Ijumaa , 7th Apr , 2017

Mazoezi ya mashindano ya Formular 1, Chinese GP yameshindwa kufanyika leo, na kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya kwenye mji wa Shanghai, China.

 

Waandaaji wa mashindano hayo, wamepanga mazoezi hayo, kufanyika kesho, ingawa hakuna uhakika kama fainali yake inaweza kufanyika Jumapili kama ilivyopangwa.

Mazoezi hayo yalisimamishwa zikiwa zimebaki dakika 20 timu ziingize magari kwenye barabara, kutokana na helicopter kushindwa kutua kwenye hospitali za karibu za kutoa huduma pindi inapotokea ajali, kwa sababu ya utando wa wingu zito, mjini Shanghai.

Kama hali ya hewa ikiendelea kuwa hivyo, kuna uwezekano kesho kukafanyika mazoezi na fainali, ili kuepuka hali mbaya ya hewa ambayo inategemea kurejea Jumapili, siku ya fainali Chinese GP.

Dereva wa Mercedes Mwingereza Lewis Hamilton, yeye aliandika kwenye Twita kuwa ni bora kungefanyika mazoezi Jumamosi mara tatu, na Jumapili asubuhi, ingefanyika fainali.