Aggrey Morris
Morris alipata majeraha hayo wakati Azam FC ikiichapa Mbabane Swallows bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo katikati ya wiki iliyopita alianza na programu ya mazoezi ya ‘gym’ kabla ya kuhamia uwanjani.
“Nashukuru Mungu kwa kuweza kurejea uwanjani kwani lengo langu ni kucheza na siyo kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kwani hakuna kitu kibaya kwa mchezaji kama kupata majeraha yatakayomuweka nje ya uwanja kipindi kirefu sana” Alisema Morris
Beki huyo amerejea wakati Azam FC ikiwa kwenye maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Yanga, utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wikiend hii (Jumamosi) majira ya saa 10.00 jioni.