
Nancy Sumary
Akizungumza leo katika kilele cha kuazimisha siku ya mwanamke duniani mrembo huyo amesema pedi pekee yake haitoshi kumaliza au kutatua tatizo hilo kwa watoto wa kike bila ya kushirikishwa Wizara ya Elimu kwa lengo la utoaji elimu kwa jamii nzima ili watambue thamani ya mtoto wa kike.
"Mimi binafsi ninawathamini wasichana 50 ili waweze kuhudhuria vipindi vyao kiufasaha shuleni lakini pedi haitoshi peke yake kuwa suluhisho ya tatizo hili inapaswa wizara ya elimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watoe elimu elekezi na siyo kwa wasichana tu, bali mpaka kwa wavulana ili tatizo liweze kutatulika kuanzia chini". Alisema Mrembo huyo
Kwa upande mwingine Nancy ameitaka jamii kumthamini mtoto wa kike kwa kumpa haki zake zote kama anavyopewa mtoto wa kiume.
Utafiti uliyofanywa na baadhi ya mashirika ya kutetea haki za mtoto wa kike zilibaini asilimia kubwa ya watoto wa kike wanashindwa kufanya vizuri masomo yao wakiwa shule kutokana na ukosefu wa pedi pindi wanapoingia hedhi jambo linaloisukuma EATV Ltd kuanzisha kampeni hiyo.
Nancy Sumari ndiye Miss Tanzania pekee hadi sasa aliyeweka historia ya kuvaa taji la 'Miss World Africa' na leo ameshiriki katka vipindi maalum vya Namthamini kwa ajili ya Siku ya Wanawake, EATV