Jumatatu , 23rd Jan , 2017

Mcheza tenisi wa Uingereza, Johanna Konta ametinga robo fainali ya mashindano ya wazi ya Australia, baada ya kumtoa Mrusi Ekaterina Makarova kwa jumla ya 6-1 6-4, huko Melbourne Park, mjini, Melbourne.

Konta (Kushoto), Serena (Kulia)

Konta mwenye umri wa miaka 25, sasa atakutana na kigogo wa tenesi Mmarekani, Serena Williams ambaye naye ameshinda 7-5 6-4 dhidi ya Barbora Strycova kutoka Jamhuri ya Czech.

Naye Mcroatia Mirjana Lucic-Baroni alimaliza kiu yake ya kusubiri kwa miaka 18 kutinga robo fainali kwa mashindano ya Gland Slam, baada ya kupata ushindi dhidi ya Mmarekani Jennifer Brady

Lucic-Baroni, mwenye umri wa miaka 34, alishinda kwa seti mbili za  6-4 6-2 na kutinga robo fainali kwa mara ya kwanza tangu atolewe na  Steffi Graf  kwenye mashindano ya Wimbledon mwaka 1999.