Jumatano , 7th Dec , 2016

Msanii ambaye ni rapper wa muziki wa bongo fleva Young D au paka rapper, amesema Tuzo za EATV (EATV AWARDS 2016) zimempa ari ya kuzidi kufanya kazi kwa bidii zaidi, ili mwakani aweze kushiriki.

Msanii Young D (katikati) akiwa na watangazi wa kipindi cha 5SELEKT, Tbway 360 na Vanila

 

Akizungumza kwenye kipindi cha 5SELEKT cha East Africa Television kilichoruka moja kwa moja kutoka Mlimani City jijini Dar es Salaam, Young Dee amesema baada ya kuona hamasa ya mwaka huu, mwakani anajipanga ili awe miongoni mwa washiriki.

"Unajua siku zote tuzo zinaleta recognition kwenye kazi za wasanii, zinaleta hamasa, na mimi mwakani nitaongeza bidii kwenye kazi zangu, kwa sababu najua mwisho mwa mwaka kuna kitu kama hiki cha tuzo", alisema Young Dee.

Young Dee ambaye mwaka huu alipata matatizo baada ya kujiingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na kuamua kuacha bila kulazimishwa, amekuwa ni msanii anayejitahidi kurudi kwenye game, kwa kuachia kazi tofauti tofauti ikiwemo kazi yake ya sasa ya furaha.

Tags: