Jumanne , 13th Mei , 2014

Baada ya taarifa kusambaa kuwa msanii wa Kenya aliyejipatia umaarufu kwa kushinda taji la Tusker Project Fame, Ruth Matete amefilisika kwa kumaliza mamilioni ya pesa alizoshinda kama zawadi, msanii huyu amerejea katika muziki na ngoma ya injili.

Tusker Project Fame

Ruth tayari amekwishaungana na Spotlight Media kwa ajili ya kutengeneza video ya kazi hii mpya, huku akiwa chini ya makubaliano ya kufanya kazi na timu hii kwa kipindi cha miaka miwili zaidi.

Kuhusiana na suala la yeye kuishiwa, msanii huyu amesema kuwa, hizi ni tetesi zinazosambazwa na watu walio karibu yake ambao wana lengo la kumuangusha na hazina ukweli wowote.