Jumanne , 22nd Nov , 2016

Msanii wa taarabu Black Kopa amesema wimbo wake unaofuatia utakuwa ni remix ya wimbo wa kaka yake Omary Kopa ili kuweza kumuenzi katika muziki wake.

Black Kopa

 

Hata hivyo Black Kopa amesema kuamua kurudia wimbo wa kaka yake haimaanishi kwamba ameishiwa  nyimbo za kuimba ila anafanya hivyo kuonesha mapenzi kwa kaka yake japo muda unambana  kwa kuwa na yeye ana nyimbo zake zote ambazo anatarajia kuziachia hivi punde.

Akiongea ndani ya eNewz amesema ameamua kuurudia wimbo huo kwa kuwa alikuwa akiuimbia katika majukwaa mbalimbali na mashabiki kumshauri aurudie na pia ameahidi kurudia nyimbo zote za kaka yake kwa muda tofauti hivyo mashabiki waendelee kumsapoti katika kazi yake.