Alhamisi , 10th Nov , 2016

Mwili wa aliyekuwa Spika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samwel Sitta unatarajiwa kuwasili leo mchana ukitokea ujerumani ambapo umauti ulimkuta alipokwenda kupatiwa matibabu.

Marehemu Samwel Sitta

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia yake imeeleza kuwa mwili wa Sitta utapokelewa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Baada ya kuwasili kwa mwili huo baadaye upelekwa katika ukumbi wa karimjee kabla ya kupelekwa Dodoma kwa ajili ya kuagwa na wabunge kabla ya kusafirishwa kupelekwa Mkoani Tabora kwa ajili ya maziko siku ya Jumamosi.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu baada ya kuhani msiba huo Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Rajab Luhwavi amesema Sitta ametekeleza majukumu yake mbalimbali kitaifa kwa uwezo mkubwa.