Alhamisi , 20th Oct , 2016

Msanii wa filamu nchini Rammy Galis amefunguka na kusema kuwa historia ya wazazi wake kidogo ni changamoto na kudai kuwa katika kipindi chote cha maisha yake hajawahi kumuona wala kuonana na baba yake mzazi.

Rammy Galis

 

Rammy Galis alisema hayo kupitia kipindi cha KIKAANGONI kinachuruka LIVE kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi jioni, Rammy Galis alidai kuwa yeye amelelewa na baba yake wa kambo ambaye pia amekwishafariki.

"Unajua historia ya wazazi wangu kidogo ni changamoto mama yangu yeye ni Msomali na baba yangu alikuwa ni mtu wa Brazil, baba alikuwa baharia hivyo sijawahi kumuona wala sijawahi kuonana naye, kwa hiyo mimi nimelelea na baba yangu wa kambo ambaye naye baadaye alikuja kufariki" alisema Rammy Galis 

Mbali na hilo Rammy Galis anadai kwa sasa ameamua kuweka cheti chake cha 'Degree' ya kwanza pembeni na kufanya kazi za jamii, ikiwemo sanaa ya uigizaji, kufanya biashara za magari pamoja na kufanya kilimo cha bustani.