
Ally Mabuyu (kushoto)kutoka jijini Dar Es Salaam na Juma Yusuph (kulia) kutoka Zanzibar wamepata nafasi ya kwenda Brazil kupata mafunzo ya soka na kushuhudia uzinduzi wa kombe la dunia.
Vijana wawili zao la kopa Cocacola, Ally Mabuyu kutoka jijini Dar Es Salaam na Juma Yusuph kutoka Zanzibar wamebahatika kupata nafasi ya kwenda nchini Brazil kushuhudia ufunguzi wa kombe la dunia. Wakiongea mbele ya waandishi wa habari mara tu baada ya kutambulishwa, vijana hao wamesema huo ni mwanzo wa kutimia ndoto zao za kufanikiwa katika soka na kuchezea timu ya taifa.
Aidha mwakilishi wa shirikisho la soka duniani FIFA Bwana Henry Tandau amesema FIFA kwa kushirikiana na washirika wake wana miradi mbali mbali ya kuukuza mchezo huo na kuigusa jamii pamoja na kutengeneza maisha ya baadaye ya watoto.