
Kiyoyozi
Hatua hiyo imechukuliwa ili kutekeleza mkataba wa kimataifa wa kutunza tabaka la O-ZONE linaloharibiwa kutokana na ongezeko la kemikali hizo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira kutoka ofisi ya makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi amesema wanahitaji kujua takwimu za kiwango cha matumizi ya vifaa vinavyoingizwa nchini ili kuwawezesha kuweka namna ya kudhibiti uingizwaji wa bidhaa hizo.
“Tumewashirikisha wadau ambao kwa kiasi kikubwa watatuwezesha kujua ni kiasi gani kuna matumizi ya kemikali hizo na baadaye tutakuja na mpango kazi wa namna tutakavyo washirikisha wadau na wananchi katika kuzuia kemikali hizi.
Washiriki katika kuandaa takwimu hizo wameishauri serikali kudhibiti uingizwaji wa majokofu, viyoyozi vya zamani ili kuwalinda wananchi wake dhidi ya madhara.