Baadhi ya vijana wanaochukua mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa.
Hayo yamebanisha na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini (JKT), Brigedia Jenerali Michael Isamuyo, katika hotuba yake iliyosomwa na mwakalishi wake Kanal John Mbung'o katika sherehe za vijana zaidi ya 1000 kuhitimu mafunzo ya kuruta.
Brigedia Jenerali Isamuyo amesema kuwa itakuwa ni fedheha kwa taifa ikibainika kuwa vijana hao waliopikwa kwa misingi ya uzalendo wameshiriki katika matukio ya ujangili na migomo vyuoni isiyo na tija au kutumika kisiasa.
Kwa upande wao vijana hao waliohitimu mafunzo hayo wamewataka vijana kushirikiana na serikali katika kudumisha amani ya nchi mshikamano na kutumia changamoto kuwa fursa za kuwaletea maendeleo.