Muonekano wa sehemu ya Jiji la Mwanza
Hali hiyo imetokana na kugundulika kwa wanafunzi wa kike watano wa kidato cha kwanza wa shule hiyo, kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa walimu aliyekuwa akifanya mafunzo ya vitendo.
Wazazi ambao watoto wao wanadaiwa kuhusika na tuhuma hizo ambao wamefika katika shule hiyo wamewasilisha kilio chao kwa serikali na kutaka tabia hiyo ikomeshwe.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamelaani kitendo cha mwalimu huyo ambaye ni mwanafunzi kutoka chuo cha Tumaini tawi la Makumila.
Mkuu wa shule hiyo, Boniface Mjuli, amesema amelazimika kuwaita wazazi hao na kuwataka kwenda shuleni hapo na vipimo vya afya za watoto wao baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mzazi mmoja ambaye binti yake anahusika na mahusiano ya kimapenzi na mwalimu huyo ambaye kwa sasa anafanyiwa uchunguzi.
Kamati ya nidhamu ya shule hiyo inalifanyia uchunguzi suala hilo kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.