
Mkurugenzi wa shirika linalotetea maslahi ya watu wenye ulemavu wa ngozi la Under the Same Sun, tawi la Tanzania, Vick Mtetema (kulia), akiwa na meneja uendeshaji wa shirika hilo Gamariel Mboya. UTSS limekuwa mstari wa mbele katika utetezi wa haki za watu wenye ulemavu wa ngozi.
Akizungumza kwa niaba ya Rais Kikwete katika Maadhimisho ya Tisa ya Siku ya Albino Tanzania Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii nchini Dk. Seif Rashid amesema chini ya muongozo huo watu wenye albinism wataweza kuhudumiwa maradhi ya saratani huku akisisitiza hospitali za serikali kutambua umuhimu wa muongozo huo pale utakapokamilika.
Kwa upande wake, msomaji wa risala katika maadhimisho hayo kwa niaba ya watu wenye albinism Bw. Hussein Kibinda ameitaka serikali kufanya utafiti wa kubaini ukubwa wa tatizo la saratani kwa watu wenye albinism hapa nchini.