Alhamisi , 1st Mei , 2014

Msanii wa muziki wa miondoko ya Reggae na R&B, Pius Mayanja maarufu zaidi kama Pallaso ambaye makazi yake ni huko Marekani, ametua nchini Uganda kwaajili ya kutoa shavu katika onyesho kubwa la uzinduzi wa albam mpya ya Radio na Weasela hapo kesho.

Pallaso

Palasso ambaye kipindi cha nyuma alikuwa akifanya kazi chini ya lebo ya Leone Island ya Jose Chameleone, kwa ujio huu anatarajia kuleta ladha na burudani aina yake, hasa pale atakapofanya live ngoma ya Amaaso aliyofanya pamoja na Radio na Weasel.

Pallaso pia anatarajia kutumia ziara hii kufanya kolabo kadhaa na wasanii wa uganda kabla ya kurejea tena marekani.

Tags: