Jumatatu , 25th Jul , 2016

Soko Kuu la Kariakoo linatarajia kukusanya Shilingi Milioni 60 hadi 70 kwa mwezi kama wafanyabiashara wote ndani ya soko hilo watalipa kwa wakati ushuru na fedha hizo kuelekezwa katika uboreshaji wa miundombinu ya soko hilo.

Akiongea na East Africa Radio kaimu Meneja wa soko la Kariakoo bwana Mrero Mgheni amewataka wafanyabiashara walipe kodi kwa wakati ili kuhakikisha utaratibu huo unafabyika kwa wakati.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa soko hilo wamelalamikia utaratibu uliowekwa na uongozi wa wilaya ya Ilala wa kukataza magari ya bidhaa kuingia ndani ya soko hilo kwa kuwa wanapata changamoto kubwa yakupata bidhaa hizo kwa sasa.

Akitolea ufafanuzi wa jambo hilo Bwana Mgheni amesema wameanza mazungumzo na wahusika ili kuangalia namna yakutatua tatizo hilo kwakutenga eneo maalumu lakushushia bidhaa hizo na kuwafikia wafanyabiashara hazo kwa uharaka.