PIPI NA MUMEWE
Pipi alisema kwa sasa yeye ni mama wa watoto wa wili na aliamua kuachana na maisha ya bata na kuanzisha familia yake kwani maisha ya bata huwa siku zote sio mazuri na pia anasema tangu ameolewa ameenelea kuwa mzuri zaidi kwa kuwa hana mawazo kabisa.
Pia Pipi alikuwa na aliwasihi wasanii wa Bongo sasa hasa kina dada na wale hasa wanaotafuta kiki na kutegemea kiki ziwatoe kimaisha kuwa kwa ufupi huwa kiki zinampoteza msanii katika fani yake na si kumpa mafanikio kwa kuwa zinawashushia heshima zao katika jamii.
Hata hivyo pipi alimalizia kwa kusema nyimbo zake zote ambazo amekua akiziimba especially zile alizoandika mwenyewe amekuwa akiimba sehemu kubwa ya maisha yake anayoishi kila cku huku akisema muziki unachangamoto saana na unapaswa kuuona kama kazi yako ili uweze kukulipa vizuri.



