Alhamisi , 30th Jun , 2016

Stand United imeamua kumuongeza mkataba wa miaka miwili, Haruna Chanongo huku ikiongeza wachezaji wengine wapya wakiwemo kutoka nje ya Tanzania kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Orodha kamili ya wachezaji hao ni kama ifuatavyo Yusuph Sabo(Coastal union), Hassan Mpilipili (Toto Africans), Jerome Sina (Rayon Sports ya Rwanda),
Nurdin Mganga (Mgambo Jkt), Benedictor Jacob (Lupopo fc-Congo), Hassan Salum (Coastal union), Mussa Kirungi (Toto African) na Saleh Abdallah (Kagera Sugar).

Wengine Jamal Mchauro (Azam fc), Sami Ally Nuhu(JKU-Zanzibar), Fehi Abdulrahman (Mafunzo-zanzibar), Hassan Salum (Simba SC), Zablon Anatai (Kagera Rangers) pamoja na Najim Salum(Changanyikeni fc).

Kikosi cha Stand United kinaingia katika kambini rasmi Julai Mosi jijini Dar es Salaam.