Kikosi cha Medeama ya Ghana katika picha ya pamoja.
Sare hiyo unawafanya wawakilishi wa Tanzania Young Africans kushika nafasi ya mwisho katika kundi hilo baada ya kupoteza michezo yake miwili ya awali walipofungwa na MO Bejaia kwa bao moja kwa sifuri na juzi kupokea kipigo cha idadi hiyo hiyo kutoka kwa TP Mazembe ya DR Congo.
Yanga italazimika kushinda mechi ijayo dhidi ya Medeama mchezo utakaopigwa Julai 15 katika uwanja wa Taifa siku ambayo MO Bejaia itakua inacheza na vinara wa kundi hilo TP Mazembe.
Nayo Klabu ya soka ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imeifunga Enyimba ya Nigeria mabao 2-1 mjini Pretoria katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika siku moja baada ya vigogo wengine wa Afrika Al Ahly kuambulia kichapo nyumbani dhidi ya Asec Mimosas.
Kabla ya mchezo huo Sundowns waliwafunga Entente Setif ya Algeria 2-0 lakini mchezo huo ukatangazwa batili baada ya Setif kushindwa kuwazuia mashabiki wao kufanya fujo.
Ushindi huo unaipa Sundowns alama sawa na Zamalek katika kundi B timu zote zikiwa na ushindi wa mchezo mmoja huku zikiwa zimesalia timu tatu katika kundi hilo.



