Jumatatu , 28th Apr , 2014

Katika kuelekea kwenye kilele cha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani wadau wa tasnia ya habari nchini Tanzania wameandaa maadhimisho ya siku mbili yatakayofanyika mjini Arusha ili kuibua changamoto zinazoikumba tasnia ya habari.

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika moja ya majukumu yao ya kila siku

Jaji mstaafu na aliyewahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali Jaji Mark Bomani anatarajiwa kuongoza maadhimisho hayo yatakayoanza Mei mbili na kumalizika Mei nne mwaka huu.

Akizungumzuia maadhimisho hayo, afisa kutoka Baraza la Habari Tanzania - MCT, Bw. Allan Lawa amesema MCT itazindua machapisho matatu ikiwa ni pamoja na lile litakalokuwa na ripoti ya hali ya vyombo vya Habari nchini kwa mwaka jana.