Jumapili , 19th Jun , 2016

Kipa wa Simba, Peter Manyika (Jr), amesema ndoto zake ni kuwa kipa mkubwa nchini kama baba yake, Manyika Peter, na kwamba anaamini ipo siku ataitwa Tanzania One.

“Mimi bado mdogo, sema nimeanza kucheza timu kubwa mapema, na hilo ndilo limefanya niwe na jina kubwa mapema na ukizingatia nimerithi mikoba ya baba yangu, ambaye alikuwa kipa namba moja nchini enzi zake,”

“Mwaka huu nilitarajia sana kuanza kuwa kipa wa kudumu wa Taifa Stars baada ya kufanya vizuri nikiwa na timu zote za vijana, lakini nafikiri sikuwa na msimu mzuri sana pale Simba, ndiyo maana sikufikiriwa Taifa Stars, ila sasa ninajipanga upya,” alisema.