Ijumaa , 25th Apr , 2014

Msanii wa muziki Jaguar kutoka nchini Kenya, alilazimika kuondolewa jukwaani katikati ya onesho mjini Nakuru hivi karibuni kutokana na mashabiki wa msanii huyu kuzua tafrani ambayo ilitishia kutokea kwa uharibifu wa mali wakati akitoa burudani.

Jaguar

Tukio hili limeripotiwa kusababishwa na kitendo cha msanii huyu kutoa pesa na kuwarushia mashabiki hawa, na kuwafanya kupagawa wakati kila mmoja akijaribu kupigania bahati ya kuokota pesa hizo.

Katika ufafanuzi wa msanii huyu baada ya kitendo cha kuondolewa jukwaani, Jaguar amesema kuwa alikuwa akijaribu kujichanganya na kufurahi na mashabiki wake, na kushushwa kwake jukwaani ilikuwa ni kwasababu ya usalama wake, kwa vile ingewezekana sana kwa mashabiki hawa kumvamia na kumwibia.

Tags: