
Yang Feng Glan ama Malkia wa Pembe za Ndovu
Kesi inayomkabili raia wa China ajulikanaye kwa jina la Yang Feng Glan maaarufu kama Malkia wa Pembe za Ndovu, anayekabiliwa na mashitaka ya kufanya biashara haramu pembe za ndovu imeahirishwa tena hii leo kufuatia Mkurugenzi wa Mashitaka DPP kuomba fursa ya kufanyika uchunguzi zaidi.
Yang Feng Glan ama Malkia wa Pembe za Ndovu nchini Tanzania amefikishwa leo kwenye Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam akiwa na washitakiwa wengine wenzake wanaokabiliwa na kesi hiyo ya kufanya biashara haramu ya pembe za ndovu kesi.
Wakizungumzia kesi hiyo mawakili wa serikali Paul Kadushi na Faraja Nchimbi wamesema upelelezi wa kesi hiyo ulikwisha kamilika lakini Mkurugenzi wa Mashitaka DPP ameona kuna baadhi ya maeneo yanatakiwa kufanyiwa uchunguzi zaidi.
Raia huyo wa China aliyekamatwa kwa makosa ya biashara haramu ya pembe za ndovu zenye thamani ya dola milioni mbili na nus, ambapo kwa mara ya kwanza alifikishwa katika mahakama hiyo Oktoba 12 mwaka jana. Kesi hiyo imehairishwa na itatajwa tena Juni 20 mwaka huu.