Jumatano , 1st Jun , 2016

Msanii Bounako amabye anaunda kundi la N2N soldiers kutoka pande za Arusha, ameamua kugeukia shughuli ya uchimbaji wa madini, katika mgodi huko Mererani.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Bounako amesema ameamua kuingia kwenye madini kwanza ili kusaka mkwanja mkubwa, kwani alikuwa na ndoto hiyo siku nyingi.

“Ni Kweli nipo mgodini na nikweli sasa hivi nafight na game stone, kwa sababu nina big dream dream kwenye maisha yangu, always nina big dream ya kufikiria B5, kwa hiyo sasa ndio life style yangu ndo mana nipo napambana, na naona mwanga kwa hiyo nina imani saa yoyote nitakuwa Zimba”, alisema Bounako.

Pia Bounako amezungumzia kuhusu kundi lao la N2N Soldiers na kusema kuwa kundi hilo bado lipo halijafa, na anaamini wenzake wana uwezo wa kusimama bila yeye na kuiwakilisha N2N.

“N2N soldier mtu mmoja ni kama band, bado tutawatesa na bado tutaspend hata line zenyewe zinajionyesha, kichwa chochote cha Nako 2 Nako kina uwezo wa kuhold solo artist , lakini hata wenzangu wakitoa ngoma nisipokuwepo nafurahi naona wenzangu dah wameniwakilisha”, alisema Bounako.