Jumapili , 8th Mei , 2016

Wanawake wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), wamesema kuwa licha ya kesho kurejea katika vikao vya bunge baada ya kususia ila msimamo wao wa kujiondoa katika umoja wabunge wanawake upo pale pale.

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Halima Mdee

Akizungumza na East Africa Radio Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Halima Mdee, amesema kuwa tayari wameshaandika barua kwa Naibu Spika kuhusiana na suala hilo na wanasubiri maamuzi yake.

Mhe. Halima Mdee amesema kuwa wameamua kufanya hivyo baada ya kuona umoja huo ambao ulitakiwa kukemea matendo ya udhalilisha kwa wabunge wanawake haujalipa uzito wa suala hilo ambalo limeelekezwa kwa wabunge wanawake wa vyama vya upinzani.

Mhe. Mdee amesema kuwa hatima yao ya kurudi katika umoja hou wa wabunge wanawake itategemea na Naibu Spika ambae pia ni kiongozi katika umoja atajibu nini na baada ya hapo watakaa kujadili ni jinsi gani wataweza kushirika katika umoja huo.