Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa, Crispin Luanda akisalimiana na Waziri Jummanne Maghembe
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa, Crispin Luanda, kufuatia muitiko mdogo wa Jamii katika kutumia huduma za uzazi wa mpango hasa kwa wananchi wenye maisha ya hali ya chini.
Mkurugenzi huyo aliyazungumza hayo katika kata ya Nyehunge ambapo mamia ya wakazi wa Kata hiyo walijitokeza kupata elimu ya uzazi wa mpango iliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Maria Stopes.
Bw. Luanda amesema kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka tofatui na mtarajio ya taifa ya kiuchumi hasa kwa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na kusema kusema suala hili linafanya wazazi wengine washingwe kumudu gharama za maisha.
Amesema idadi ya watu lazima iwiane na ukuaji wa uchumi au na uwezo wa serikali kuhudumia wananchi wake kwa hiyo changamoto kubwa kama watu watakuwa wengi zaidi ya serikali kuwa na uwezo wa kuwahudimia hali ambayo itafanya huduma ya wananchi kuwa hafifu.
Halmashauri ya wilaya ya Buchosa inawakazi zaidi ya lakini moja na elfu hamsini ambao ni asilimia kumi na sita tu wanatumia uzazi wa mpango