
Kizito Mihingo
Mihigo pamoja na wenzake wawili wanatuhumiwa kushirikiana na waasi wengine wa kabila la Kihutu kutoka huko Afrika Kusini na Dr Kongo katika njama za kupanga mashambulizi kwa ajili ya kuiangusha serikali.
Hata hivyo ripoti nyingine zinamtaja Mihigo kama mtu ambaye alikuwa karibu zaidi na chama tawala cha Rwandan Patriotic Front (RPF), na kukamatwa kwake kumekuwa jambo ambalo linashtusha wengi.