Jumanne , 12th Apr , 2016

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa ameipongeza timu ya

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa, Kassim Majaliwa ameipongeza timu ya mpira wa miguu ya Namungo FC na kuikabidhi zawadi ya sh. milioni tano baada ya kuibuka mabingwa wa ligi daraja la tatu mkoa wa Lindi.

Ubingwa huo wa mkoa ulionyakuliwa na timu ya wilaya ya Ruangwa, umeiwezesha kupanda daraja la pili taifa, hivyo watapata mechi zitakazochezwa nyumbani na ugenini.

Timu hiyo iliyoanzishwa na wafanyakazi wa mgodi wa Green Ganet uliopo Namungo, kijiji cha Chingumbwa wilayani Ruangwa, mwaka huu imekuwa mabingwa wa ligi daraja la tatu mkoa wa Lindi hivyo kupata tiketi ya kucheza ligi daraja la pili ngazi ya taifa.

Akipokea kombe hilo jana Waziri Mkuu, Majaliwa amesema amefurahishwa na ubingwa huo, ambapo amewataka wadau wa soka wilayani humo kuiunga mkono timu hiyo na kuhakikisha inapanda daraja na kucheza ligu kuu ya soka Tanzania bara.

Pia amesema atafanya mazungumzo na halmashauri kuona kama wana eneo kwa ajili ya kujenga kiwanja cha mpira wa miguu na litakapopatikana wananchi wanaweza kuanza kujenga mabanda ya biashara kuzunguka kiwanja hicho na kisha kutafuta mfadhili kwa ajili ya ujenzi wa eneo la kuchezea.