Katibu wa Wizara ya maliasili na Utalii, Meja jenerali Gaudence Milanzi,
Katibu Mkuu huyo ametoa kauli hiyo Jijini Arusha, wakati wa mkutano wa pili wa wadau wa masuala ya utaliii hapa nchini ambapo amesema serikali ipo katika jitihada za ya kupambana na ujangili kwa kuanzisha awamu ya pili ya Operesheni tokomeza ambayo itakuwa tofauti na ile ya awali.
Amesema mfumo wa oparesheni ya sasa itaanzia katika namna ya uajiri wa askari, mafunzo ya askari hali itakayofanya opresheni hiyo kufanyika kwa kuzingatia haki na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tofauti na ile ya mwanzo iliyokuwa na matatizo.
Aidha amesema katika kuhesabu pembe za ndovu zilizopo kutafanyika ukaguzi wa pembe hizo zilizopo kwenye maghala na sio kutokomeza ili kujua idadi kamili ya nyara hizo za serikali na kuepusha udanganyifu wa baadi ya watu kujifanya wamezitekeza nyara hizo kumbe na wao wanachukua na kwenda kuziuza.
Kwa upande wake mkurugenzi wa hifadhi za taifa (TANAPA), Alan Kijazi amesema wamejipanga kueleza mikakati ya shirika kwa wadau wa utalii ili waweze kukubaliana mbinu za kuongeza utalii nchini.