Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Arusha Neema Mollel,
Utalii huo wa Baiskeli ambao ni wa kipekee umekua kivutio kwa watu wengi na unatarajia kuwa chachu ya watalii wengi kutembelea hifadhi hiyo yenye wanyama pori aina ya pundamilia,tembo,nyati na faru pamoja na maporomoko ya maji na ziwa momela.
Afisa Masoko na Utalii wa Hifadhi hiyo Jerome Ndazi Akizungumza na Waandishi wa Habari waliokuwa kwenye ziara ya kutembelea vivutio vya utalii kwa lengo la kutangaza utalii na kuhamasisha utalii wa ndani iliyoandaliwa na TANAPA,Jerome Ndazi amesema kuwa tayari maandalizi ya kuanzisha utalii kwa njia ya baiskeli umekamilika na kwa sasa wako katika hatua za mwisho za kukamilisha na kuanza rasmi.
Kaimu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Arusha Neema Mollel, amesema kuwa tayari wmeshaandaa njia za utalii wa baiskeli ambazo zitatofautiana na za utalii wa kutembea kwa miguu hivyo watanzania na wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi kutembelea hifadhi hiyo yenye vivutio vingi katika eneo dogo ikiwemo wanyama,maporomoko ya maji na milima.
Hifadhi ya Taifa Arusha (TANAPA) ilianzishwa mwaka 1960,ukubwa wa eneo la uhifadhi hivi sasa ni kilomita za mraba 322 likijumlisha Mlima Meru wenye urefu wa mita 4566 juu ya usawa wa Bahari .