Jumatano , 3rd Feb , 2016

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa idadi ya watu, UNFPA limesema mpango wa miaka kumi wa harakati za kutokomeza ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake, FGM nchini humo umekuwa na mafanikio.

Mtaalam wa Masuala ya Idadi ya Watu toka UNFPA, Bibi Christine Mwanukuzi-Kwayu (Kushoto) akizungumza wakati alipofuatana na Kaimu Mwakilishi Mkazi wa UNFPA

Mwakilishi msadizi wa UNFPA nchini humo Christine Mwanukuzi-Kwayu amesema kuwa mila hiyo inahusisha sherehe na kupakwa poda badala ya kukeketwa ambapo wasichana zaidi ya 400 wameepushwa kukumbana na ukeketwaji na kupatiwa mila mbadala.

Na kama hiyo haitoshi wavulana nao wanasaidia dada zao katika kampeni hiyo akigusia kwenye kongamano moja ambapo vijana wamejitokeza kuwatetea wasichana katika kupinga kwa nguvu unyanyasaji huo.

Kwa mujibu wa mwakilishi msaidizi huyo wa UNFPA Tanzania, mikoa mitano ndiyo inaongoza ambayo ni Manyara, Dodoma, Singida, Arusha na Mara ambapo mkoani Manyara wanawake 81 kati ya kila 100 wamekeketwa.
Sambaza.