Nyota wa muziki nchini Inspekta Haroun 'Babu'
Babu amesema kuwa safari zake Afrika Kusini zinakuwa ni moja kati ya jitihada kuhakikisha kuwa licha ya ukongwe katika fani, hapitwi na muda.
Inspekta amesema kuwa, kutokana na fursa nyingi za kupiga hatua kimataifa kupatikana Afrika Kusini, amekuwa nchini huko kujifunza mambo mengi kati ya hayo, kutokana na kutaka muziki wake kufika mbali zaidi ya alipoweza kuufikisha sasa.