Jumanne , 5th Jan , 2016

Waziri wa maliasili na utalii Prof. Jumanne Maghembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa mipango na matumizi endelevu ya raslimali za misitu, Mohammed Kilongo na mawakala wa huduma za misitu nchi nzima kwa kushindwa kusimamia mapato ya serikali ipasavyo

Prof. Maghembe ametoa agizo hilo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na wanahabari, kusema kuwa amefikia uamuzi huo baada ya kubaini kuwa maofisa hao wa wilaya na mikoa hukusanya mapato ya misitu lakini fedha hizo hua hazifiki katika mfuko mkuu wa Taifa.

Hata hivyo Maghembe ameagiza maofisa wa wilaya wa misitu kwa muda wa siku kumi wakusanye mapato yatokanayo na misitu na fedha hizo, wapeleke benki na watunze vitabu vya ushahidi na asiyefanya hivyo kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Misitu ni moja kati ya raslimali kubwa ambayo ipo Tanzania ambapo ikitumiwa vizuri katika ukusanyaji wa mapato yake, fedha zake zinaweza kusaidia kutatua kero mbalimbali za wananchi