Ijumaa , 25th Dec , 2015

Star wa muziki wa bongofleva nchini Best Nasso ambaye sasa amekuja kivingine akielekeza zaidi uwezo wake katika mahadhi ya Rhumba ameamua kutoa zawadi ya funga mwaka kwa kuachia video yake mpya inayoitwa 'Rhumba'.

Staa wa muziki wa bongofleva nchini Best Nasso

Best Nasso ameongea na enewz kuhusiana na wimbo huo ambao umeongozwa vyema na Kenny, amesema kuwa pamoja na kuachia video hiyo anaamini kuwa hii ni moja ya hatua nzuri kuelekea kimataifa huku akiwashi mashabiki kutoa sapoti na kuipokea kazi hii mpya.