Jumatatu , 21st Dec , 2015

Bobi Wine, ameomba ruhusa kwa mamlaka inayoendesha Jiji la Kampala KCCA kumpatia kibali cha kuingia mstari wa mbele na kuchukua jukumu la kutengeneza barabara iliyopo huko Kira ambayo imekithiri kwa ubovu ikisababisha kero mbalimbali kwa wananchi.

Bobi Wine (aliyevaa koti jekundu) akiwa ameingia barabarani kufanya marekebisho

Hatua hiyo imekuja baada ya Bobi Wine kujaribu kuanza kuitengeneza wiki kadhaa zilizopita, hatua iliyovuta mamlaka hiyo kuleta vifaa na kuanza kuitengeneza ambapo hata hivyo kazi hiyo ilisimama bila kukamilika na kusababisha kero zaidi.

Bobi ambaye anafahamika kama Rais wa Ghetto amesema kuwa, kitendo cha KCCA kutelekeza bara bara hiyo hususan katika msimu huu wa sikukuu kimezua kero zaidi, akiamini kuwa akiachia jukumu hilo sambamba na wananchi, watakamilisha kazi hiyo kabla ya sikukuu ya Krismasi.

Tags: