Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy
Akiongea na East africa radio leo Meneja mawasiliano kutoka Mamlaka ya mawasiliano nchini Bw. Innocent Mungi amesema kuwa baada ya kutambulishwa kwa mfumo huo serikali inatoa miezi sita kwa watumiaji wa simu feki na zisizokidhi viwango, kununua simu nyingine kwa kuwa baada ya hapo watazifunga
Bw. Mungi amesema zaidi ya Asilimia 60 ya Watanzania wameanza kutumia mfumo huo mpya na kugundua ubora wa simu wanazonunua na kuwataka watanzania watumie vizuri mfumo huo ili kuepuka hasara pamoja na kulinda simu zao na wizi wa simu za mkononi.
Aidha Bw. Mungi amesema kuwa endapo mtu atatoa taarifa ya kuibiwa kwa simu yake kituo cha polisi na kwa mtoa huduma basi simu hizo zitafungwa kufanya kazi huku akibainisha kuwa na huo ndio utakua mwisho wa wizi wa simu za mkononi kwa Tanzania.