Jumanne , 15th Dec , 2015

Michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea hapo kesho kwa kupigwa mchezo mmoja ambapo mabingwa watetezi Yanga watakutana na African Sports ya jijini Tanga katika mchezo utakaopigwa Uanja wa Mkwakwani jijini humo.

Kwa upande wa Vinara wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara Azam Fc inatarajiwa kuelekea Mjini Songea siku ya Ijumaa kwa ajili ya maandalizi ya mechi yake dhidi ya Majimaji itakayipigwa mwishoni mwa wiki mjini humo.

Akizungumza na East Africa Radio Afisa Habari wa Azam Fc Jaffer Iddy maganga amesema, kikosi kimeingtia kambini hapo jana na kocha Mkuu wa Timu hiyo Stewart Hall anaendelea kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo wao dhidi ya Simba Sc ili kuweza kupambana na kupata Pointi Tatu na kuendelea kukaa kileleni mwa Ligi.

Maganga amesema, katika mechi hakuna mchezo mrahisi hivyo anaamini mchezo huo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kujipanga lakini wao kama Azam Fc kila mechi kwao ni fainali hivyo watajitahidi mpaka kuweza kufikia malengo.