Kikosi cha timu ya Vijana ya Ilala kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mchezo wao na Boom FC katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Benjamini Mkapa ..
Mwenyekiti wa chama cha soka la Vijana manispaa ya Ilala Edwin Mloka maarufu kama Father amesema maandalizi ya mtanange huo yamekamilika na tayari kila kitu kipo kwenye utaratibu wake kuhakikisha bingwa wa mwaka huu anapatikana .
Mloka ameongeza kuwa wao kama viongozi wamefurahishwa kwa namna vijana wanavopata fursa ya kuonesha vipaji vyao kwenye mashindano kama hayo ambayo ana imani yana manufaa kwa manispaa yao na nchi kwa ujumla.
Amewataka viongozi wa vyama vya soka mikoa mbalimbali nchini kuhamasika na kuandaa mashidano kama yao ili waweze kuibua vipaji kwenye maeneo yao kutoka kwa vijana ambao wamekuwa hawapati nafasi ya kucheza kwenye mashindano makubwa.