Mwanariadha huyo mlemavu sasa anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp mwaka 2013, hukumu ambayo inatarajiwa kutolewa mapema mwakani.
Pistorius alimuua mwanamitindo Reeva Steenkamp siku ya wapendanao kwa kumpiga risasi nne zilizopenya kwenye mlango wa choo uliofungwa na kumpata akiwa ndani.
Kwa sasa Pistorius alikuwa anatumikia kifungo cha nyumbani baada ya kukaa jela kwa mwaka mmoja katika adabu ya kifungo cha mwanzo cha miaka mitano.