Jumapili , 22nd Nov , 2015

Vyombo vya ulinzi na usalama jijini Dar es Salaam vimeagizwa kuanza mara moja kufanya uchunguzi, kuhusiana na kifo cha aliyekuwa msemaji wa chama cha Madereva nchini Bw. Rashid Saleh

Vyombo vya ulinzi na usalama jijini Dar es Salaam vimeagizwa kuanza mara moja kufanya uchunguzi, kuhusiana na kifo cha aliyekuwa msemaji wa chama cha Madereva nchini Bw. Rashid Saleh, kutokana na kifo chake kutokea katika mazingira yenye utata na yanayozua maswali mengi.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda, ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam leo, wakati wa maandalizi ya safari ya mazishi ya kiongozi huyo, yaliyokuwa yakifanyika katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, ambapo amesema taarifa za madaktari zinasema figo zilishindwa kufanya kazi na jitihada zilifanywa ili kutatua tatizo hilo.

Akimzungumzia Bw Saleh Makonda amesema kuwa alikuwa ni shujaa na mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya madereva hasa katika kutetea mikataba na haki za madereva nchi nzima na kuwa jitihada nyingi zimefanyika katika kuokoa uhai wake

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Madereva Bw. Shaban Mdemu amekihusisha kifo cha marehemu Saleh kuwa kina uhusiano na harakati zake za kudai haki kwa madereva