Staa wa muziki wa dansi kutoka Kongo, Ferre Gola
Hili linakuwa ni tukio kubwa kabisa na la kwanza katika eneo hilo la Afrika Mashariki toka kuanza kwake kufanya muziki binafsi baada ya kuacha kufanya kazi na Koffi Olomide na Clinton Kalonji.
Nyota huyo amesema kuwa, ujio wake Kenya ni maalum kwaajili ya kukidhi kiu kubwa ya mashabiki wa muziki wa lingala ambayo wapo nayo tokea kipindi soko lilipokuwa limetawaliwa na Koffi Olomide na Zaiko Langa Langa, kufikia sasa ambapo ndio wakati wake.
Nyota huyo ambaye kipaji chake kimegunduliwa na nyota mkongwe wa muziki huo, Werrason Wenge Musica, amekuwa akiwekeza nguvu kubwa katika kazi zake tokea kuanza mpaka sasa ambapo ana albam zipatazo 12 zinazofanya vizuri.