Spika wa bunge la Tanzania Bi. Anna Makinda akiwa na Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa kuuaga mwili wa Mrehemu Deo Filikunjombe
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika mazishi ya Mbunge huyo Spika Makinda amesema kuwa Filikunjombe alikuwa ni mpiganaji kwa kufanya kile anachokiamini na kuikosoa serikali pindi inapokwenda tofauti pamoja na huhakikisha wananchi wanapata haki zao.
Amesema kuwa wananchi wamempoteza mpigania haki zao na wakakikishe kuwa wanaangalia mbunge atakeye kuwa tayari kumalizia mipango aliyokuwa ameianza mbunge huyo.
Aidha kwa upande wake Rafiki yake mpendwa wa Fili kunjombe, Kiongozi wa Chama cha ACT wazalendo, Zito Kabwe, amesema kuwa anasikitika kutokea kwa msiba wa rafiki yake huyo na kuwa hatoweza kumpata rafiki wa aina ya Filikunjombe kutokan ana alivyokuwa.
Amesema kuwa kwa wakazi wa Ludewa wamempoteza mtu muhimu sana na kuwa hawatampata mbunge kama huyo licha ya kuwa watapata mbunge lakini hawezi kufanana na Deo.
Akihubiri katika ibada ya mwisho ya msiba wa marehemu watatu ambao ibada ilikuwa ni moja Askofi wa Kanisa la Romani Katoliki jimbo la Njombe, ask. Alfred Maluma alisema kuwa msiba huo ni mkubwa kwa kuwa umehusisha watu watatu wanaotokea sehemu moja na kuwatia moyo wafiwa kwa kuwaambia kuwa wawe wavumilivu katika siku hizi ngumu kutokana na msiba wenyewe ulivyotokea na ughafla wake.
Katika msiba huo kuna viongozi mbalimbali walifika kuomboleza akiwemo Mkuu wa mkoa wa Njombe Dr. Rehema Nchimbi, Waziri wa maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu, Wiliamu Lukuvi, na viongozi wengine wa chama cha mapinduzi wa nyazifa mbalimbali.