Jumapili , 18th Oct , 2015

Jeshi la polisi,Tume ya taifa ya uchaguzi NEC na ile ya Zanzibar ZEC, wametakiwa kutumia busara katika kuamua faida na hasara za watu kubaki umbali wa mita 200,kutoka vituo vya kupigia kura ili kuepusha nchi kuingia katika machafuko yasiyo na ulazima

Mratibu wa Taifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa

Ombi hilo ni sehemu ya maazimio yaliyomo ndani ya Tamko la Asasi za Kiraia, lililotolewa jijini Dar es Salaam leo baada ya kukamilika kwa mkutano mkuu wa baraza hilo, ambao ulikuwa unajadili viashiria vya uvunjifu wa amani na hatua zinazostahili kuchukuliwa, ikiwa imebaki juma moja kabla ya siku ya kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu.

Akisoma sehemu ya tamko hilo, Mjumbe wa baraza hilo Bw. Deus Kibamba amesema ni bora wananchi wakaruhusiwa kufuata utaratibu uliozoeleka miaka katika chaguzi zilizopita.

Naye Mjumbe mwingine Bw. Onesmo Olengurumwa yeye akiiomba mahakama isaidie kutoa tafsiri ya kisheria ili kumaliza mvutano wa umbali gani mwananchi anastahili kukaa mara baada ya kupiga kura huku viongozi wastaafu wakitakuwa kuwa washauri wa vyama vya siasa kwa kutokuegemea upande wowote.