
Msanii mkongwe wa muziki nchini Mzee Ally Zahir Zorro
Gwiji huyo ambaye ni mkongwe katika tasnia ya muziki nchini ameeleza kuwa kukosekana kwao kutumbuiza katika kampeni zinazoendelea ni kutokana na kukosa ukaribu na waratibu wa kampeni husika.
Mzee Zorro ameeleza kuwa, amekwishawahi kushiriki katika shughuli za kampeni kipindi cha nyuma, ingawa sasa shughuli zake za bendi zimemuweka mbali na majukwaa hayo, akieleza kuwa licha ya hali ya mambo kwenda tofauti atatoa ushirikiano kwa Rais ajaye bila kinyongo.
