Ijumaa , 28th Mar , 2014

Ostaz Juma Namusoma, msimamizi wa wasanii ambaye naye pia ameingia katika game ya kurap, ameamua kutolea ufafanuzi taarifa swala zima la mahusiano yake ya kimapenzi kwa sasa.

Hii ni kufuatia taarifa mbalimbali za kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na msanii wa filamu Bongo, Blandina Changula, maarufu zaidi kama Johari.

Ostaz ambaye tayari ana mke kwa sasa, kuhusiana na swala la yeye kuwa katika mahusiano na Johari na kutaka kumuoa ndani ya siku za usoni, amekubaliana na taarifa hizi na kuhusiana na yeye kumuoa Johari, na kusema mapenzi yao yalianza zamani na sasa wapo katika mipango ya kufunga ndoa.

Ostaz amesema kuwa, kwa sasa wapo katika mipango ya kumbadilisha dini Johari kuwa muislamu tayari kabisa kwa kufunga naye ndoa kama mke wa pili kitu ambacho ni halali kabisa katika dini ya kiislamu.

Msikie hapa Ostaz akizungumza mwenyewe katika mahojiano yake na eNewz kuhusu ishu hii.