Mwenyekiti wa kamati ya ufundi ya Chama cha Wavu Mkoa wa Dar es salaam DAREVA, Nassoro Sharif amesema, ligi hiyo itashirikisha timu 42 kati ya hizo zikiwemo timu 10 za wanawake ambapo upande wa wanaume timu zitagawanywa kwa makundi manne wakati zile za wanawake zikiwa katika makundi mawili.
Sharif amesema, ligi hiyo inalengo la kutafuta timu ya mkoa ambapo miaka ya nyuma timu ya mkoa ilikuwa ikipatikana kwa utaratibu wa kutoa nafasi kwa timu kutoa wachezaji ambao walikuwa wakifanya vizuri katika vilabu vyao.



