Jumatatu , 14th Sep , 2015

Ally Baucha, msanii wa muziki na mtayarishaji katika tasnia ya Bongofleva, ameweka wazi juu ya ujio wa uhakika wa umoja wa wasanii kutoka kusini mwa Tanzania - Kusini All Stars.

Ally Baucha, msanii wa muziki na mtayarishaji katika tasnia ya Bongofleva

Kama sehemu pia ya mchango wake katika kuunganisha nguvu kupeleka muziki mbali, Ally Baucha ameeleza kuwa
wameamua kujipanga sasa kutokana na umuhimu wa ushirikiano katika mpango huo, nia ikiwa ni kuinua wanamuziki na muziki kutoka kanda hiyo ya Tanzania ambayo bado ipo chini.