Jumamosi , 12th Sep , 2015

Wachezaji Mohammed Hussein 'Tshabalala' wa Klabu ya Sima, Haji Mwinyi wa Yanga na Shomari Kapombe wa Azam Fc wametakiwa kuzitumia vizuri nafasi walizonazo katika vilabu vyao ili kuweza kufika mbali zaidi kisoka.

Mchezaji wa zamani wa Klabu za Simba na Yanga Ramadhan Wasso amesema wachezaji hao wanaocheza nafasi za beki katika vilabu vyao wanatakiwa kujitambua na kurekebisha makosa madogo waliyonayo ili kudumu katika nafasi adimu walizonazo kwa hapa nchini.

Wasso aliyekuwa akiitumikia nafasi ya beki wa Kushoto amesema wachezaji nchini wanatakiwa kujithamini na kuachana na mambo yatakayoweza kuchangia kushusha kiwango chao cha soka walichonacho hivi sasa.