Twiga Stars iliyochini ya Kocha Rogasian Kaijage inaingia Uwanjani baada ya kupoteza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Ivory Coast kwa kufungwa bao 1-0 ikiwa kundi A.
Kwa matokeo hayo, Twiga Stars inashika nafasi ya tatu katika kundi lake linaloongozwa na Nigeria iliyoifunga mwenyeji wa mashindano hayo Congo mabao 4-1 katika mchezo wake wa awali.
Baada ya mchezo wa leo, Twiga Stars itabakiwa na mechi moja kukamilisha ratiba dhidi ya wenyeji Congo ambao watakutana Septemba 12 na baada ya mechi hiyo itajulikana kama itaendelea au itarejea nyumbani.