Jumamosi , 29th Aug , 2015

Squeezer, nyota kongwe katika tasnia ya Bongo Fleva amewatoa wasiwasi mashabiki kuwa hataacha nafasi ndefu ya ukimya tena, sababu iliyomuweka pembeni kwa muda ikiwa ni kuweka sawa mambo ya kifamilia akiwa kama kaka mkubwa baada ya mzee wake kufariki.

Squeezer

Baada ya kuvunja ukimya jana na kutambulisha pini jipya, mwambie kupitia show ya Planet Bongo East Africa Radio, ikiwa pia wiki kadhaa zimemalizika akiwa na project mpya mkononi, hapa anakiri kutoitendea haki game yake kutokana na safari nyingi kwenda mkoani Mbeya na pia Dar hapa kuhakikisha shughuli za kifamilia zinakaa sawa sawa.

Star huyo pia akagusia suala la joto la kisiasa ambalo linahisiwa na kila mtanzania sasa na kusema kwa upande wake anaona ni vigumu kufahamu ni nani ataibuka mshindi katika kinyanganyiro cha uchaguzi mwisho wa mwezi wa 10, akitaka watanzania kutulia na kutumia busara kupima uwezo wa kiongozi wa kweli na kusimamia amani ambayo ndiyo kitu muhimu cha kudumisha.

Tags: